Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-, Uongozi wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran umesema kuwa operesheni ya Mersad itaendelea kuwa alama ya mamlaka na nguvu ya Iran, pamoja na mfano wa msimamo thabiti wa wananchi wa nchi hiyo katika kulinda ardhi yao.
Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu, kwa mnasaba wa kumbukumbu ya operesheni hiyo, Jeshi la Iran limesema kuwa tarehe 5 Mordad (27 Julai) inawakilisha ukurasa wa dhahabu katika historia ya mapambano na ustahimilivu wa wananchi wa Iran.
Taarifa hiyo imesisitiza kuwa Jeshi na Vikosi vya Wanajeshi vya Iran viko katika hali ya tahadhari ya kudumu kwa ajili ya kukabiliana na adui, na kwamba uchokozi wowote dhidi ya nchi hiyo utakabiliwa kwa nguvu kubwa na jibu kali zaidi.
“Tutamzuia na kumwangamiza kila mvamizi atakayethubutu kugusa hata chembe moja ya ardhi ya taifa letu,” ilisema taarifa hiyo.
Jeshi la Iran limeeleza kuwa Operesheni ya Mersad iliibua msukumo wa kitaifa miongoni mwa wananchi wa Iran wa kukabiliana na uchokozi wa adui, na kuwa mfano wa mshikamano kati ya wananchi na Vikosi vya Wanajeshi katika medani ya mapambano.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, operesheni hiyo, iliyotekelezwa chini ya mkakati madhubuti wa kijeshi wa Shahidi Luteni Jenerali Ali Sayyad Shirazi na kwa kutumia uwezo mkubwa wa kijeshi katika uwanja wa mapambano, ilisababisha moja ya ushindi mkubwa zaidi katika historia ya Ulinzi Mtakatifu, na kuwapatia washambuliaji kushindwa vibaya.
Uongozi wa Jeshi la Iran umehitimisha kwa kusisitiza kuwa Operesheni ya Mersad ni ukumbusho wa uwezo wa Iran wa kulinda mamlaka yake na ardhi yake, huku ukionya kwamba uchokozi wowote wa baadaye utakabiliwa na jibu kali, zito na la kuamua.
Maoni yako